Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Matumizi ya Wedi 95 na kuendelea sehemu ya kwanza

Utangulizi juu kutumia Kurasa za Microsoft Word 95 na kuendelea

[Introduction to Using Word 95 and later ]

Sehemu ya kwanza

Kurasa za Microsoft wedi (word) za kuanzia mwaka (95/97/98/2000)na kuendelea ni mfumo wa maandishi (word process) ambao unatumika kama mfumo maalumu wa uendeshaji shughuli za uandishi wa maneno na nyaraka mbalimbali. Wedi (word) inayotumika kuunda/kuandikia, kuhariria, kuchapishia nyaraka mbalimbali.

Matumizi mengi ya kurasa hizi za microsoft ambazo hutumika huwa na mfumo unaokaribia kufanana kabisa na hivyo huwa rahisi kwa mtu yeyote kuwa akijifunza mojawapo ya kurasa hizi za programu ya wedi huwa tayari anaweza kutumia zilizobakia mfano: Mtu akijifunza microsoft wedi ya mwaka 97 anaweza pia kutumia microsoft wedi ya mwaka 95/98/2000/2002 na kuendela japo kutakua na nyongeza ya vikorombwezo ila zile programu za msingi hubakia kuwa zilezile tu. Pia unapokuwa umejifunza programu moja kama vile wedi (word) ni rahisi kwako pia kujifunza programu mfano: ekseli-spredishiti (spreadsheet package Excel) au aksesi-databezi (the database package Access).

Katika mafunzo haya ya wedi (word) tunachukulia kuwa wewe tayari unafahamu matumizi ya vitu kama mausi (mouse) na kuwa unaufahamu wa kutosha kuhusu kurasa za microsoft kama tulivyojifunza katika mafunzo ya awali.


Kufungua wedi (Starting Word)

Kufungua Wedi (word), bonyeza kwenye kitufe cha kuaza Anza (Start) kwenye Task Bar. Bonyeza kwenye progamu halafu bonyeza Microsoft Word.

Skrini (The screen)

Skrini ya Word imegawanyika katika sehemu mbalimbali kama inavyoonekana hapa chini:

Unapoandika maneno juu ya hii skrini yanaingizwa kwenye ukurasa huu.

Andika sentensi mbili au tatu. Utagundua jinsi ambavyo maneno yakizidi kwa mbele moja kwa moja hurukia mstari unaofuata kwa chini. Bonyeza kitufe kilichoandikwa Ingiza/Ingia (Enter) kwenye kiibodi ili kuanza aya mpya.

Kionesheo (kasa/cursor

Kionesheo (cursor) huwakilishwa na ishara ya alama I ambayo inakuwa inachezacheza na kadri unavyoandika kinasogea mbele.

Elewa kuwa pale kinapokuwapo ndipo ambapo ukiandika kitu kinajiandika nakuwa ukitaka kuhama kwenda kuandika au kurekebisha sehemu fulani inakubidi uhamishe kiongozeo/mausi (Mouse) hadi pale unapotaka kuandika au kurekebisha na kisha ubonyeze kiongozeo chako na kile kionesheo kitaonekana pale. Baada ya kukiona andika au fanya marekebisho unayotaka kufanya.

Namna ya kuchagua/How to select

Ilikuweza kuchagua waraka au maneno fulani kwa ajili ya kuyafanyia kazi unapasawa kufanya yafuatayo.

Weka mausi pale unapotaka kuanzia kuchagua kisha bonyeza shikilia na kisha buruza bila kuachia hadi pale unapotaka kuishia .hapo maandishi yatakuwa yamebadilika rangi na kuwa na rangi nyeusi kuashiria kule kuchagua na baada ya hapo unaendelea na kile ulichokusudia kama ni kuboldi kuandalaini au kukopi.

Sogeza Kiongozeo/mausi (mouse) kusogeza kionesheo/kasa (cursor) ilikufikia sehemu unayotaka kufuta na kisha utumie kitufe kilichopo kwenye kiibodi kilichoandikwa Kurudisha nafasi nyuma (backspace) kufuta sehemu unayotaka. kwenye kiibodi yako katika vitufe vya kati kuna kitufe kimoja ambacho ni kirefu kuliko vingine vyote, hiki kinaitwa SPACE BAR .



Kazi ya kitufe hiki ni kusogeza nafasi pale mtu anapokuwa anaandika ili herufi zisisongane .

  • Upande wa katikati kuna kitufe kingine kinachoitwa DELETE



    hiki kazi yake ni kufuta maandishi yote yale ambayo utakuwa umeyachagua. Ilikuchagua maandishi inabidi ubonyeze sehemu ya maandishi ambako unataka kuanzia kuchagua kisha uburuze bila kuachia hadi utakapofikia pale mwisho wa pale unapohitaji kufuta.

    Baada ya kuchagua maandishi hubadilika kuwa meusi na endapo utabonyeza delete au backspace basi maandishi yote yatafutika.

    Njia nyingine ya kuchagua maandishi ni kubonyeza sehemu kulikoandikwa edit kisha uchague neno select all kisha urudie tena kubonyeza view, halafu neno delete. Tatizo la njia hii huwezi kuchagua kifungu cha maneno bali ni lazima uwe unania ya kufuta kila kitu.

    Kwa kusogeza kiongozeo peke yake hakufanyi sehemu yoyote ile isogee bali unatakiwa pia uboinyeze sehemu mpya unayotaka kuandika ili kuhamishia kionesheo/kasa (cursor) na hivyo upate kuandika.

    Ili uweze kuchagua/kuainisha kwa nia ya kufute au kusogeza maandishi inabidi ubonyeze bila kuachia na uburuze hadi mwisho wa neno la mwisho unalotaka kufuta baada ya hapo bonyeza kitufe cha kwenye kiibodi kilichoandikwa futa diliti (delete) au bakispesi (backspace). Pia unaweza kuandika unachotaka kuandika na yale uliyokwishayachagua yatafutika mara moja. Sasa jaribu kuchagua na kuandika kisha utagundua yale maandishi uliyochagua yamefutika/deleted na nafasi yake kuchukuliwa /replaced na yale unayoyaandika.

    Sehemu kinapokuwa kichwa cha habari/Title bar

    Mstari wa juu ya Skrini unajulikana kama Mstari wa kichwa cha habari/Title bar. Huonyesha jina la ukurasa unaouangalia/unaoutumia kwa wakati huo mfano(Microsoft Word) na jina la nyaraka/waraka unaoutumia. Kama hakuna ukurasa ulioufungua basi kichwa cha habari au faili lililofunguliwa basi hujiandika Waraka wa kwanza/Document1.

    Rudi Juu/Top of document



    Orodha ya yaliyomo/Menu bar

    Sehemu inayoonyesha yaliyomo/Menu bar ni orodha ya inayoonyesha yale ambayo mtu anaweza kuyachagaua au kuchagua moja mabalo anataka kulifanyia kazi au kuliangalia kwa mfano; Kufungua word.

    Kwa kubonyeza Sehemu ya yaliyomo/menu huweza kupata orodha ya majina au vitu vipatikanazo kwenye huo ukurasa kwa kwenda chini.

    Kwa kubonyeza kwenye mstari wa kichwa cha habari Title bar utaweza kufunga orodha ya yaliyomo/menu bila kuathiri kazi au waraka unaokuwa unatumia au kuandika.

    Kama mstari/rula haionekani unaweza kuifungua kwa kwenda kwenye kitufe kilichoandikwa angalia/rula/View/Ruler kisha ukibonyeze na mara rula itatokea
    (Zingatia/note: rudia hatua hii na uchague kuficha rula/hide ruler iliuifiche kama huihitaji).

    Kuna njia fupi ya kufanya baadhi ya mambo yani (sortcuts)Some commands have shortcut zinazofahamika au ambazo ni muhimu kuzifahamu:

    Bonyeza sehemu iliyoandikwa faili/file ilikupata orodha/menu. Tazama
    Ctrl+S: pembeni ya neno tunza/Save
    na Ctrl+P: pembeni ya neno chapa/Print.


    Unaweza kutumia njia fupi kama njia mbadala wakati wa kufanya kazi zako.

    Baadhi ya vibonyezeo huwa na vidotidoti/ellipsis kama hivi (...).Hivi humaanisha kwamba pale utakapo vibonyeza kisanduku cha maelezo kitajitokeza ilikukupa maelezo ya jinsi ya kufanya.



    Rudi Juu/Top of document


    Tuli baazi/Toolbars

    Toolbars ni vitufe vyenye picha ambavyo huwakilisha vitufe vinginevyo (icons au Vibonyezeo/buttons) kwa ajili ya kutumiwa na kiongozeo/mausi (mouse). Kwa kubonyeza kwenye kimojawapo ya kitufe kunamaanisha kuamuru au kuelekeza jambo fulani lifanyike.

    Kuweza kupata au kujua matumizi ya kila kitufe haswa vile vinavyokuwepo juu ya kurasa unapofungua, pitisha kiongozeo/ mausi (mouse) kisha utaona kile kitakachojiandika pale kumaanisha kazi ya hicho kitufe (hiki huitwa vidokezo vya maelezo ya kwenye skrini/ScreenTips).

    Hivi vibonyezeo huonyeshwa kwenye
    standadi /standard na
    fomatini/formatting tuli baa/tool bars kutegemeana na uelekeo na saizi ya programu za kiofisi unayoitumia.
    Hizo tulibaa huwa zinawekwa kiupande upande ilikubana nafasi.
    Kuweza kupata vitufe au batani za ziada bonyeza palipoandikwa tools kisha bonyeza neno option halafu chaguaVitufe zaidi/More buttons button




    Standadi tuli baa/Standard Toolbar

    Standadi tuli baa/standard toolbar hii hupatikana chini ya menu baa/menu bar.



    Kwa watumiaji wenye ujuzi wa kutosha au uzoefu wanaweza kuongeza vitufe au batani ila haifai kumruhusu mtu yeyote yule tu achezee au kubadili kitu chochote bila ya wewe mwenyewe kuelewa kile anachokibadilisha na kuwa umeridhika nae.

    Rula (Rulers)

    Chini ya fomatini tuli baa kuna rula iliyokaa kiulalo ikionyesha mistari ya pambizo.

    Rula iliyokaa ulalo/Vertical Ruler Hii inakuwepo upande wa kulia wa ukurasa ikiwa wima.




    Sikroli baazi/Scroll bars

    Skroli baa ya ulalo na ile iliyokaa wima hutumika pamoja na mausi/kiongozeo kusogeza waraka wowote ule ambao upo kwenye skrini kutoka juu kwenda chini na vilevile kutoka chini kwenda juu.

    Kwa kubonyeza vijimishale vilivyoko kwenye skro baa kunawezesha waraka au kazi yako kutoka chini kwenda juu au kutoka juu kwenda chini na vivyo hivyo kwa upande wa ulalo ambapo inatoka kushoto kwenda kulia na kutoka kulia kwenda kushoto. Pia waweza kuburuza sehemu ya kati ya skroli baa ili kusogeza kazi yako upande uitakayo.


    Sehemu ya urefu ya skroli baa huonyesha ni sehemu gani ya waraka/kazi ambayo inaoyeshwa katika sehemu ya maandishi. Kwa mfano: kama kimshale cha kwenye skro baa kipo nusu ya ukurasa inamaanisha kuwa sehemu ya maandishi nayo yapo nusu.



    Statazazi baa/Status bar

    The Tatazi baa/Status bar hii hupatikana chini ya ukurasa na kwamba huonyesha idadi ya kurasa, idadi ya maneno yaliyokwisha kuandikwa, na namba za seksheni .



    [Back to top] [Rudi nyuma (Back)-Outlook]
    [Endelea(Next) Word2][ Rudi Kwenye yaliyomo-Contents]