

Pia unaweza kutumia *.doc kumaanisha kuwa unatafuta mafaili yote yanayoishia na neno .doc
Chini ya sehemu iliyoandikwa named unafuatia mstari ulioandikwa Containing text.katika kisanduku hiki endapo utaandika neno "kompyuta" basi utatafutiwa kila faili lililo na neno "kompyuta"
Chini ya mstari ulioandikwa Containing tex kuna mstari wa mwisho ulioandikwa "Look in".
Katika kisanduku cha mstari huo panakupa uweza wa kurahisisha utafutaji wako wa mafaili kwa kugawanya utafutaji wako kwenda kwenye sehemu mbalimbali; Mafano ukichagua C: utapata mafaili yote yaliyoko kwenye hadidiski.
Pia ukichagua My document utapata mafaili na folda zote zenye muundo wa doc pekee.
Kuyatafuta au kuyaangalia mafaili ambayo uliyatumia muda mfupi uliopita


