Matumizi muhimu yanayohusiana na Windozi 95 na kuendelea
[Using Windows 95 and later]
Faili ni nini?
Faili ni kile kinachohifadhia habari au nyaraka.
Vifupisho vya majina ya mafaili (File Extensions).
Vifupisho vya majina ya mafaili (File Extensions) ni zile herufi za mwanzo kati na mwisho wa mafaili na ambazo zinahusianishwa na mafaili yale na kuwa zinaweza kutumiwa kutafutia mafaili hayo.
Hivyo hivyo kwenye programu ya kurasa za microsoft95 na kuendelea (microsoft windows 95 and Later) huweza kutufahamisha ni programu ipi itumike au inatumika kufungulia aina fulani ya faili unalotaka kutumia.
Pia hutambulisha kuwa ni aina gani ya ya faili na la programu gani.
Kwa mfano faili lenye vifupisho .txt, ambalo lililoandikiwa kwenyeNotepad linaloitwa Namba za simu litaonekana hivi
NambazaSimu.txt ... Huhitajiki kulipa faili kifupisho cha aina hii kwani programu zenyewe moja kwa moja huyapa mafaili kifupisho.
Unahitajika tu kulipa faili lako jina na mambo mengine yatafanyika yenyewe. Vifupisho vilivyozoeleka ni hivi vifuatavyo hapa chini:
- .doc =
Microsoft Word Document
- .xls = Microsoft Excel Document
- .ppt = Microsoft PowerPoint Presentation
- .mdb = Microsoft Access Database
- .bmp = Windows Bitmap Picture
- .wav = Sound File
- .html or .htm = Internet Document
Baada ya kuwasha kompyuta yako kitu cha kwanza ambacho huonekana mbele yako ni Ukurasa/kurasa (window.
Pale ndipo hutakiwa kuanza kwa kufungua kile ambacho umekusudia mfano, kuna my computer na ukiifungua unakumbana na draivu mbalimbali draivu"A" draivu"C" draivu"E" na draivu"D".
Draivu (Drives)
Draivu (Drives)ni vifaa vinavyotumika kuhifadhia data.Kompyuta nyingi zina draivu angalau mbili:
Draivu kuu (hard drive) C:\ (ambayo ndiyo kiini cha data kuu zote) na pia flopi draivu (hii huhifadhia kiasi/kiwango kidogo cha data(1.44 Mb)ndani ya 3.5" diski - flopi diski).
Hadidraivu moja kwa moja hujulikana kama draivu C:\na ile ndogo hujulikana kama draivu A:\ au flopi diski
. Kama ukiwa na draivu ya ziada basi hiyo itaitwa flopi draivu B:\. Pia utakuwa na draivu za mtandao kutegemeana na ruhusa na haki za kila mtumiaji. Draivu hizi za mtandao zitajulikana kama draivu F:\ au H:\ au G:\. Pia kuna drive D ambayo hutumiwa kuwekea kanda za C.D za muziki au programu.
Folda (Folders)
Folda(Folders)Hutumika kupangilia data zilizohifadhiwa kwenye draivu zako ni sawa na mkoba wa kuhifadhia mafaili au droo la kupangilia mafaili. Hutumika kuhifadhia mafaili au nyaraka za aina moja kusaidia kuzitofautisha kwa kuzipa folda majina tofauti tofauti kwa umuhimu au aina ya mafaili yako.
Fikiria draivu zako kama kabati za kuhifadhia nyaraka zisizo na droo na utakapotaka kuyapangilia vyema mafaili yako ni lazima uweke droo.
Hapa unataka mafaili yenye programu za kompyuta yakae peke yake na yale yenye nyaraka fulani na kumbukumbu muhimu pia nayo yawe kwenye droo lake.
Hapa ndipo unapohitaji folda kuzipangilia na kuhifadhia kazi zako pamoja kwenye droo tofauti tofauti.Pengine utapenda kuweka mafili yanayofanana pamoja pia na kuzipa folda majina ya kipekee ili kutofautisha.
Hii picha hapa chini ni ya folda trii [folder tree] ambayo inaonyesha mtiririko na mpangilio wa folda kuu na ndogo. hii inaanzia kwenye sehemu ya kuandikia anuani ya tovuti kushuka kwenye my computer na kadhalika [address bar] kwa mfano:
Hii picha hapa chini ni ya Windozi eksiplora [windows explorer]
windozi eksiplora huypatikana kwenye programu na humwezesha mtu kufungua folda na mafaili yaliyoko kwenye kompyuta yako na pia kukuonyesha kama hili ni faili au folda nakuwa kama ni folda ni falda kubwa ambayo ndani yake zipo nyingine ndogondogo au la. Baada ya kuifungua utapata picha inayofuata hapa chini yake.
Windozi Eksiplora/Windows explorer. Hii inakuwezesha kuyaona na kuyatumia mafaili na folda zote zilizomo kwenye draivu C:
Kwenye alama za jumlisha picha ya chini inamaanisha ni folda kubwa ambazo ukizikliki tena zitafunguka na kutoa falda nyingine ndogondogo
Pia kuna folda windo mfano: my document na My Computer ambazo huweza kufunguka katika windo na kuonyesha folda zilizomo ndani yake.