Matumizi muhimu yanayohusiana na Windozi 95 na kuendelea
[Using Windows 95 and later]
Utangulizi kuhusu windozi/Introdution to Windows
Windozi ni nini?
Windozi ni kiini cha uendeshaji katika kufanya kazi na kompyuta. Ingawa zipo njia nyingine za uendeshaji mfano Apple computers hapa tutatilia mkazo windozi kutokana na kuwa ndiyo inayotumika sana hivi sasa. .
Windozi inaitwa windozi kwa sababu unaweza kuitumia kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja kwenye windo tofautitofauti.
Kwa mfano pale mtumiaji anapokuwa anasubiria windo moja ifunguke anaweza kuwa anasoma au kufanya kazi nyingine kwenye windo nyingine pia.
Hapa mtumiaji amefungua windozi zifuatazo intaneti eksiplora mbili kila moja ikiwa na ukurasa tofauti wa tovuti windo nyingine ya wedi inayoonyesha folda zilizopo na windo ya mwisho inaonyesha kikokotoleo/mashine ya kufanyia mahesabu.
Vitufe/Icons
Katika kufungua windo huwa unahitajika kubonyeza kitufeTo open windows, you usually choose an icon. Kitufe ni picha ndogo yenye maandishi chini yake. Kwa mfano hiki kitufe hapa chini kinawakilisha Internet explorer . Ukikibonyeza, windo ya Internet explorer itafunguka.
Katika skrini yako/On your screen
Katika windo 95 na kuendelea, unapowasha kompyuta yako, huwa unaona "desktopu" na "taski baa" na kitufe cha "stati/start" juu yake.
Desktop
Deskitopu ndiyo "bakigraundi". Unaweza kuona deskitopu pale ambapo hamna windo iliyofunguliwa au windo zikiwa zimefunguliwa ila zimeshushwa chini.
Taskbar
Taski baa ni baa ambayo inakuwepo chini ya skrini yako ikiwa na kitufe cha stati upande wake wa kushoto. Kwenye hiyo taski baa utaona vibonyezeo ambavyo vinaonyesha kila windo uliyofungua pamoja na vitufe vidogo vinavyoonyesha njia za makato (short-cuts) na saa.
Kitufe cha kuanzia/Start button
Unapobonyeza kitufe cha stati mfumo wa menu ambao unaonyesha na kukuwezesha wewe kuchagua mafaili unayoyataka kam vile windo unayotaka kufungua.
"Programs" -Hapa ndipo unapopata vitufe vya mafaili karibia yote ya kimatumizi utakayohitaji.
"Documents" - Hii ni orodha ya mafaili na kazi zote ulizozifanya muda mfupi uliopita na kupitia hapa unaweza kuyapata tena haraka zaidi.
"Settings" -Hii inakupa uwezo wa kufikia kontro paneli/control panel na njia nyinginezo za kuweza kubadilisha mfumo wa kimuundo wa kompyuta yako.
"Search/Find" - Hiki ni kifaa cha kutafutia mafaili.
"Help" -Hiki kinakupa msaada wa namna ya matumizi mbalimbali ya kompyuta yako.
Mara nyingi unaweza kupata vitufe vyote vya matumizi ya kompyuta yako kwenye kitufe cha kuanzia kwenye menu ya kuanzia/start menu. Pia kunakuwa na vitufe vinavyowakilisha matumizi na mafaili kwenye deskitopu na ndani ya folda (ambayo yataelezewa hapo baadaye).
Kufungua windo/Opening windows
Windo mara nyingi hufunguliwa kwa kudabokliki/kubonyeza kitufe mara mbili mfululizo bila kuachia kwenye deskitopu au kwenye menu ya kuanzia/start menu.
Kufunga windo/Closing windows
Unafunga windo kwa kubonyeza kibonyezeo kilicho andikwa "x" juu ya windo kulia.
Kubadilisha kutoka windo hadi windo nyingine/Switching between windows
Kama umefungua windo zaidi ya moja , ujue moja tu kati ya windo ulizofungua ndiyo inafanya kazi. Hii ni inamaana windo ambayo unafanyia kazi kwa wakati huo ndiyo inayofanya kazi. Kuna njia mbili unazoweza kutumia kutoka windo moja hadi nyingine na kumaanisha kufanya windo uliyokuwa hutumii uitumie na kinyume chake.
1) Unaweza kubonyeza hizo/hiyo windo nyingine kama unaiona.
2) Unaweza kubonyeza kwenye kibonyezeo kinachoiwakilisha windo unayoihitaji kwenye taski baa chini ya skrini yako.
Kupangilia windo/Arranging windows
Unaweza kusogeza windo kwa kwa kukliki kwenye taito baa/title bar kisha unaburuza kuipeleka pale unapotaka kwa kutumia mausi yako..
Unaweza kusogeza/kupunguza windo yako kwa kuweka mouse yako kwenye ncha ya windo yako hadi pale utakapoona -alama ya kijimshale mojawapo kati ya hivyo hapo pichani na kuwa kila kijimshale huelekeza upande fulani mfano kulia kushoto chini na kadhalika kisha iburuze windo yako kuelekea kule unakotaka au hadi pale autakaporidhika na saizi ya windo yako.
Minimaizini windozi/Minimising windows
Kuminimaizi windo maana yake ni kuifanya window isionekane kwa kuishusha chini kabisa ya skrini yako bila kuifunga wala kuiondoa kabisa.Unaweza kuminimaizi windo yako kwa kubonyeza alama hii hapa kwenye picha upande wako wa kushoto juu.
Maksimaizini windozi/Maximising windows
Kumaksimaizi windo maana yake ni kuikuza windo hadi ifunike skrini yote isipokuwa taski baa/task bar. Hii ni muhimu kama unataka kuona vyema kile unachokifanya kwenye windo moja unayoifanyia kazi au kusoma.
Restoarini windozi/Restoring windows
Kurestoa windo maana yake ni kurudisha windo uliyokuwa ume maksimaizi kwenye hali/saizi yake ya awali. Unaweza kurestoa windo kwa kubonyeza kwenye alama hii hapa kwenye picha.