Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Utangulizi




Kompyuta ni nini?
Swali hili lina majibu mengi kama ifutavyo:

    Kompyuta ni mashine/kifaa:-

  1. Kitumikacho katika kufanyia mahesabu, kukusanya data, vilevile hutumika kukusanya, kuweka pamoja na kuzishughulikia/kuzifanyia kazi habari hizo.


  2. Kitumikacho kuandikia kazi mbalimbali na machapisho kama vile vitabu, magazeti n.k.


  3. Itumikayo kuhifadhia kazi na habari .
  4. Itumikayo kuwasiliana na kupeleka taarifa
  5. Itumikayo kutafutia habari toka katika mitandao mbalimbali ya kimataifa kote duniani.


  6. Kwa kifupi:-

    Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wakupokea taarifa, kufanya mahesabu, kushughulikia/kufanyia kazi na kutoa matokeo ya kazi hiyo na namna ilivyondeshwa, nakutoa matokeo ya kitu kilichofanyika/kinachoonekana.

    Pia huhifadhi taarifa na kuwasiliana na watu na kompyuta nyingine. "Taarifa" inawezakuwa katika michoro, alama, nembo, tarakimu, sauti au lugha ya maandishi.
    Kompyuta imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
    1. Sehemu zisizoshikika (Software)
    2. Sehemu zinazoshikika (Hard ware)
    3. Mtumiaji (User):

      Kimsingi mtumiaji ni mtu yeyote anayetumia kompyuta, lakini kiutaalamu inaleta maana kama mtumiaji angalao awe mwenye ufahamu wa msingi juu ya matumizi ya kompyuta.

      Pia mtumiaji huwasilianana Programu (software) zilizomo ndani yake na zile programu huwasiliana na sehemu zinazoshikika (hardware) na hapo mfumo mzima wa kimatumizi hukamilika.

      Sehemu zisizoshikika
      (software)
      :
      Ni muundo wenye mfumo wa maelekezo ambao hupewa kompyuta ilikufanya kazi maalumu.

      Mfumo huu unaweza kugawanyika katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo:

      1. Mfumo wa kimatumizi (application sotfware:)

        Katika matumizi (applications) tunapata microsoft word, kwa ajili ya kuandikia barua na nyaraka mbalimbali, Excel na Access kwa ajili ya kupangilia/kuandalia data na kufanyia mahesabu.

        Hii inajumuisha Matumizi maalumu ya kiofisi (microsoft office), Mfumo wa ulipaji mishahara (payroll) na mfumo wa kihasibu (accounting system) na kadhalika.

      2. Ya pili ni muundo wa undeshaji (system software:)

        Hii inajumuisha mfumo mzima wa undeshaji katika kompyuta.
        Mfano wa mifumo (system) ni kama windows,Mac Operating System, dos.

      Sehemu zinazoshikika
      (Hardware)
      :

      Sehemu zinazoshikika (Hardware:)

      Ni aina zote za vifaa vya kielektroniki katika kompyuta.

      Kuna aina tano za vifaa vinavyoshikika:

      1. Vifaa vya kuingiza nguvu ndani ya kompyuta au kifaa chochote kitumiacho umeme (input devices) kama kibodi (keyboard), mausi (mouse) na Kipaza sauti/microphone

      2. Vifaa vya uendeshaji, kama sakiti (circuits).

        Hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho Central Processing Unit (C.P.U.) ambacho ndicho kinachounganishwa na skrini na kuwa skrini hupata maelekezo yote kutoka kwenye C.P.U.
        C.P.U. ni sehemu kuu ya nguvu za kompyuta, au kitovu cha kompyuta.

      3. Vifaa vya Kuhifadhia/kuhifadhi ni kama hadi diski/hard disk (ndani ya CPU), flopi diskifloppy diski draivu/disk drive na CD diski draivu/CD disk drive.
        Hizi zina ni sehemu zinayotunza kumbukumbu (Memory).

      4. Vifaa vya kutoa, kama Skrini/kioo cha kompyuta (screen/monitor) na Kichapishio/printer.

      5. Vifaa vya kuwasiliana kama modemu/modem na kebozi/cables.

      Utajifunza zaidi kwenye sehemu ya Vifaa.
      Kwa mifano na maelezo zaidi bonyeza hapa.

      Vifaa Vya Kompyuta

      Namna ya kuwasha na kuzima kompyuta

      1. Namna ya kuwasha kompyuta (mwanzo)

      2. Namna ya kuwasha bila kuizima kabisa

      3. Namna ya kuzima kompyuta (mwisho)

      Namna ya kuwasha kompyuta katika hatua ya mwanzo kabisa.
      Baada ya kuiunganisha kompyuta yako kwenye umeme, kilichobaki ni kuiwasha sasa.

      Mbele yako ukiwa umeketi kuielekea kompyuta yako, unakuwa unatizamana na kompyuta yako.

      Hapo unaona vitufe kadhaa ila muhimu zaidi ni kuwa kuna kitufe kimoja kwenye C.P.U na kingine kwenye Skrini/Monitor, hivi viwili ni lazima uhakikishe vimewashwa ili kompyuta yako ifanye kazi.

      Kuwasha upya Kompyuta yako
      (Restarting your Computer)


      Kuwasha upya: Hii hufanywa pale ambapo kompyuta yako inashindwa kufanya kazi vizuri au kukwama (stuck).
      Mara nyingi huwa kunakuwepo na kitufe kidogo kwenye C.P.U ambacho hutumika kuwashia upya kompyuta yako.

      Njia nyinginezo utajifunza hapo baadaye.

      Pia unaweza kubonyeza sehemu ya chini ya skrini yako, mkono wako wa kushoto kwenye kitufe kilichoandikwa Anza (Start), pale utaletewa maneno mengi chagua na bonyeza neno Zima (Shutdown) na kiboksi chenye maelezo ya jinsi ya kufanya kitatokea.

      (A Shut Down Windows dialog box will appear) Bonyeza neno zima (Shut Down), na maelezo yatakayojitokeza tena kukutaka uthibitishe kama kweli una uhakika kuwa unataka kuizima kompyuta yako au unataka kuanza upya (Restart), chagua neno Anza upya (Restart).



      Namna ya kuizima kompyuta yako:
      (Shutting Down Your Computer).

      1. Bonyeza sehemu ya chini ya skrini yako, mkono wako wa kushoto kwenye kitufe kilichoandikwa Anza (Start).

      2. Bonyeza neno Zima (Shutdown) na kiboksi chenye maelezo ya jinsi
        ya kufanya kitatokea.
        (A Shut Down Windows dialog box will appear)



      3. Bonyeza neno zima (Shut Down), na maelezo yatakayojitokeza tena kukutaka uthibitishe kama kweli una uhakika kuwa unataka kuizima kompyuta yako yatatokea.

      4. Kwenye maelezo chagua neno ndiyo/ sawa, halafu boinyeza ( yes/OK).

      5. Baada ya kompyuta yako kuzima bonyeza kitufe kikubwa cha kwenye skrini
        na cha kwenye CPU kuzima.

      6. Hapo tayari utakuwa umezima kompyuta yako kwa kufuata taratibu zilizo sahihi. Kamwe usizime kompyuta kama uzimavyo runinga yako (Televisheni)..

        Mtandao/Network

        Kama unatumia au umekuwa unatumia kompyuta katika mtandao mfanoChuoni/kazini/au taasisi za juu za elimu bonyeza hapa chini ili upate mafunzo juu ya mtandao huo

        Bonyeza hapa
        Mafunzo juu ya mtandao /Network

        [Rudi juu (Back to Top)][Rudi Mwanzo]
        [Endelea (Next)-Vifaa]