Microsoft Outlook ni programu ambayo hutumika kumsaidia mtumiaji kuwasiliana nma watu wengine kwa haraka na pia kunganisha na kuunda utaratibu wa kuwasilisha habari mbalimbali kwa watumiaji wengine. Tumia Outlook kushughulikia na kuweka pamoja ujumbe, muda wa ahadi, mawasiliano majukumu na pia kuangalizia na kufungulia mafaili mbalimbali yanayotumika kuhifadhia na kushirikiana kimawasiliano na watu wengine.
Katika Outlook, habari hukusanywa kwenye folda. Unapofungua tu Outlook kisanduku/folda chenye habari (inbox folda) hufunguka. Tumia folda ya habari kusoma na kutuma barua pepe zako na shughuli nyingine kama vile; mialiko ya vikao/mikutano, mipangilio ya kazi na maombi ya kimajukumu (inbox folda).
Kuandika ujumbe, elekezea kionesheo chako kwenye menu ya mafaili, sehemu iliyoandikwa mpya (new) na kisha ubonyeze ujumbe pepe (mail message). Ingiza/andika jina la mtu unayemtumia ujumbe/barua pepe kwenye visanduku vilivyoandikwa Kwa (To) na nakala kwa (Cc). Andika kichwa cha habari/somo ( subject of the message). Kisha andika ujumbe wako kwenye kisanduku cha maneno (text box). Unapokuwa tayari kutuma ujumbe wako bonyeza sehemu iliyoandikwa Tuma (Send).

Ilikuweza kwenda sehemu nyingine katika Outlook bonyeza kitufe cha shotikati

(click a Shortcut) upande wa kushoto wa kisanduku cha maelekezo sehemu ya kusomea na kuandika ujumbe (inbox). kwa mfano bonyeza kalenda (Calendar) ilkuweza kufungua folda ya kalenda yako.

Hapa tunaona kile ambacho tumekifungua kutoka kwenye ile shotikati/njia fupi.
Pia unaweza kutumia Outlook kama njia mojawapo ya kufungulia mafaili mengineyo kwenye hadidiski na flopidiski/draivu"A".
Ilikutizama mafaili mengine kwenye hizo sehemu zilizotajwa hapo juu bonyeza neno mengine (other) kwenye shotikati kisha ubonyeze My Computer, My Documents, au Favorites.
kama una programu ya microsoft word kwenye tarakilishi /Kompyuta yako unaweza pia kuitumia kwa pamoja na Outlook kuandika barua pepe na ujumbe mwinginw kiufundi na kwa mtindo uutakao bila wasiwasi wowote.
Ilikutumia njia hii nenda kwenye kitufe kilichoandikwa chagua ( Options) kwenye menu ya vifaa vya kuandikia. kwenye kitufe cha barua pepe chagua tumiaMicrosoft Word kama kiandikio chako cha barua pepe (Use Microsoft Word as the e-mail editor).
Kwa kutumia Microsoft Word unaweza kuandika barua pepe zako ukitumia vitu vifuatavyo;

Kisahihishi mashine (AutoCorrect).
Kama mashine husahihisha namna maandishi yatakavyotokea kwenye chapisho au kichapishio.

Namna ya kutamka neno (Spell It).
Hii husaidia kukuangalizia namna ya kutamka maneno wakati unapokuwa unaandika ujumbe wako. Pia hukuonesha kwa kupigia mstari neno lisilokuwa sahihi au lililotamkwa vibaya na kukupa maneno yanyofanana na unachokiandika iliuchague mojawapo ambalo ni sahihi.

Vitufe viainishi na namba
(Bullets and Numbering)..
Huweka vitufe viainishio na namba ilikuonyeshea mistari au ponti muhimu.

Orodha (Tables).
Autiluku (outlook) Hutumia mtindo wa orodha (tables)kuwasilisha habari katika mtindo bora kimuundo.

Kiainishi (Highlighter).
Hutumia rangi kuweka msisitizo sehemu za msingi na muhimu katika ujumbe kwa wengine wanaokuwepo hewani kwenye mtandao wakibofya (surf).

Kubadili kimuundo anuani pepe na anuani za mdahalishi
(Conversion of E-mail names and Internet Addresses).
Hii hubadilisha kimuundo majina ya anuani pepe na anuani za mdahalishi kama mashine kuwa katika viunganishi halisi (live hyperlinks) . Wedi (Word) husikani (scan) ujumbe katika maandishi ambayo yanakubalika kwenye anuani za mdahalishi mfano: www.microsoft.com au anuani pepe kama vile: watanzania@tanzania.com na kama mashine kuwa katika viunganishi halisi (live hyperlinks) .
Dokyumenti mapu (Document Map).
Hii intumika katika kuongozea na kuunganisha pamoja barua pepe zote kwa haraka zaidi. Wedi kama mashine huweza kujua kama ujumbe unahusisha mazungumzo marefu yenye msururu na hivyo kuandaa ramani ya kimuundo kupitia viunganishi na kwenda kutoka ujumbe mmoja hadi mwingine .

Kufanya marekebisho (Track Changes).
Hiki kitufe ni kwa ajili ya kuhakiki na kufanya marekebisho katika barua pepe kwa haraka zaidi.
Kwa maelezo na maelekezo zaidi namna ya kutumia Autiluku (Outlook) na Wedi (Word) bonyeza F1 kwenye kiibodi yako kisha andika swali lako katika sehemu ya kisaidizi cha ofisi halafu bonyeza tafuta (search).
Ninaamini kuwa utafurahia huduma hii na pia kuweza kufanya mambo mengi ya kiteknolojia.
[Back to top][
Rudi nyuma (Back)Anuani pepe]
[
Rudi Kwenye yaliyomo-Contents][Endelea mbele (Next)-Word1]