Mradi huu umeanzishwa na Bi. Elaine Baker, kwa kushirikiana na ndugu Peter Temu kwa nia na madhumuni ya kutaka kuwasaidia watanzania,
na jamii nyinginezo ulimwenguni ambazo zimekuwa zikishindwa kupata walau ufahamu wa msingi juu ya matumizi ya teknolojia ya kompyuta.
Mradi huu umenuia kutafsiri kozi mbalimbali zitumikazo kwenye kompyuta kwa lugha ya kiswahili na kuziweka kwenye tovuti hii.
Mategemeo na malengo yetu ni kuanza na zile kozi za msingi kabisa na kadri muda na uwezo utakavyoruhusu tutaendelea na kuongeza kozi nyinginezo kila mara.
Pia tunakaribisha maoni na pia msaada wa kutafsiri kozi kwa mtu ambaye angependa kujitolea kama sisi kwa nia na madhumuni kama yetu sisi ilikuwezesha umma wote kunufaika na ujuzi mtu huyo alioupata na angependa kuwashirikisha watu wengine.
Mtu yeyote yule anaweza kutafsiri na kututumia kwa barua pepe au sanduku la posta au kutuandikia barua pepe nasi tutamtafuta ilikupata huo msaada wake kwa kozi atakayokuwa ametafsiri au ushauri juu ya kuboresha mradi na tovuti kwa ujumla.