Kiunganishi (Hyperlink)
Kiunganishi (A Hyperlink) Ni kiunganishi katika hali ya maneno au picha ambacho ukikibonyeza hukupeleka katika ukurasa wa tovuti au hukupeleka kwenye tovuti nyingine.
Ni sawa na chombo cha usafiri kwani hukusafirisha toka sehemu moja kwenda nyingine.
Viunganishi hivi huwa na rangi tofauti mara nyingi na kuwa unaweza kuvifahamu pale tu utakapopitisha au utakapoweka kiongozeo/mausi (mouse) chako juu maandishi yake au picha na kutazama, pia huwa vimepigiwa mistari.
Kiunganishi pia hutambuliwa kutokana na kujitokeza kwa mkono pale unapogusisha kasa/kionyesheo (cursor) kwenye kiunganishi chochote.
Sehemu unayotaka kufungua au sehemu ambako kiunganishi hicho kitakupeleka huonekana sehemu ya chini ya ukurasa.
Tazama kwenye hii picha hapa chini. Hii picha kwa chini inaonyesha kuwa kiunganishi hiki kitakupeleka kwenye;
file:///C:/WINDOWS/Desktop/Tovuti mpya/vifaa.html.
Hiki kiunganishi kinatokana na sehemu ulipo mkono: yaani sehemu iliyoandikwa chini ya ukurasa, na pale utakapobonyeza kiunganishi hiki utapelekwa au utafungua sehemu ya chini ya ukurasa huo.
HTML
HTML - ni lugha inayotumiwa kuandika programu za madahalishi/kipeperushi na ndiyo inayotumiwa kutengenezea kurasa za tovuti. Idadi kubwa ya kurasa unazoziona kwenye kipeperushi zimeandikwa kwa lugha hii (HTML).
Rudi juu (Back to Top)
Kutafuta kwenye madahalishi/kipeperushi (Searching the Internet).
Kuna mitambo mingi ya kutafutia vitu mabalimbali kwenye madahalishi/kipeperushi.Mitambo hii huwa inakuwezesha wewe uandike neno lolote, au kifungu fulani cha maneno/picha /habari na wenyewe kukutafutia ndani ya mamilioni ya tovuti zipatikanazo kwenye madahalishi/kipeperushi duniani kote.
Hapa chini kuna orodha ya mitambo maarufu ya kutafutia inayopatikana kwenye kipeperushi.
" Bonyeza kwenye kichwa cha habari mojawapo cha mitambo hiyo iliupelekwe kwenye tovuti ya mtambo husika."
- Kwa mfano unaweza kutafuta picha mbali mbali za viongozi watu au vitu fulani.
- Pili unaweza kutafuta neno moja kwa uhakika zaidi kwa kuandika neno hilo kisha kuongeza neno na (and).
Mfano pale unapotaka kutafuta neno kilimo ila ukimaanisha kilimo cha Tanzania unatakiwa kuandika KILIMO NA (AND) TANZANIA AU KILIMO +TANZANIA.
Hii itamaanisha kuwa unatafuta kilimo maneno yaliyona kilimo Tanzania au Tanzania kilimo.
Hii inarahisisha wewe kupata kile unachokitafuta badala ya kuletewa neno kilimo kutoka sehemu zote zile duniani.
Altavista
Altavista ni mtambo maarufu wa kutafutia ambao unaweza tu kuingiza neno au kifungu cha maneno juu ya kile unachokitafuta.
Altavista inakuruhusu pia kutafuta kwa kutumia vipengele mabalimbali.
Mfano:kutafutia picha na habari mbalimbali.
Kwa kutumia sehemu ya msaada (help) katika mtambo huu utaweza kupata maelekezo ya msingi juu ya namna ya kuafuta kwenye mtandao wa kipeperushi kwa ufanisi zaidi.
Kwenye mtambo wa altavista ilikutafuta kifungu cha maneo katika hali halisi tumia alama za kufungulia usemi na kufungia usemi.
mfano: maneno kama "shule/vyuo" huwa yanpewa umuhimu na maana ileile sawa na shule vyuo au "shule vyuo".
Pia ni vyema kuandika neno lenye ukamilifu mfano; Dar-es-salaam badala ya Dar-es-salaam pekee ambapo yatatafutwa hata maneno ambayo hayaihusu Tanzania unamaanisha Dar-es-salaam ya Tanzania pekee.
Pi mtambo wa altavista hutafsiri maneno na vifungu vya maneno kwa lugha mbalimbali zijulikanazo ulimwenguni. Mtambo huu unauwezo wa kutafsiri hadi maneno 150 kwa mara moja tu.
| Ukiandika Neno |
Utatafuta na kupata |
Shule na Vyuo
Shule / Vyuo | Maneno yote yanayoanza au husu shule na vyuo. |
Kilimo na (and ) Tanzania au Kilimo / Tanzania | Hii itamaanisha kuwa unatafuta maneno yaliyona kilimo Tanzania au Tanzania kilimo. |
Bill | Utapata maneno au majina yote yale ambayo yanaanzia na Bill duniani kote. |
Bill na America | Utaletewa maneno au majina ya Bill yapatikanayo America pekee. |
Altavista!
google

Kufungua au kuingia katika mtandao wa mdahalishi/kipeperushi.
Ila kwa mtumiaji/watumiaji wa kompyuta kwenye internet cafe hawana haja ya kuwaza juu ya njia ipi ya kuunganishwa kwenye mtandao wa mdahalishi/kipeperushi.
Pia wao hawana shida ya kujiuliza jinsi ya kufungua kompyuta kwa sababu vyote hivyo huwa vinafanywa na wahudumu wa kwenye internet cafe.Wewe kazi yako huwa ni kutumia tu.
Ila kuna kitu cha umuhimu kukifahamu nacho ni kitufe/Aikoni (icon)

Ukibonyeza kwenye hiki kitufe moja kwa moja itakufungulia ukurasa wa kwanza ambao utakuwezesha wewe kuandika anuani ya tovuti unayotaka kufungua.
Kwa mashirika, makampuni na taasisi mbalimbali kama vile vyuo huwa wanapeana namba za siri na majina ya kipekee ili waweze kutumia mtandao wa mdahalishi/kipeperushi au komputer hizo.
Hii inatokana na hali halisi kuwa watumiaji ni wengi na sio vyema ziachwe bila kufungwa hivyo.
[Rudi juu (Back to Top)][Rudi nyuma(Back)Mdahalishi-1]
[Endelea(next)-Anuani Pepe][Rudi Mwanzo wa Tovuti]