Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Anuani ya Barua Pepe

Anuani ya Barua Pepe (E-mail Address)

Utangulizi (Introduction):

Niimani yangu kubwa kuwa Barua pepe na ambayo inatumia mfumo wa kielekroniki kwa hivi sasa ina thamani kubwa na kuwa inaelekea kutawala kabisa njia nyingine za mawasiliano.

Barua pepe ni rhisi na haraka kulikoni barua za kupitia posta. Hazina usumbufu na mshutuko kama simu,hazina ugumu na gharama kama faksi (kinakilishi).

Kwa kutumia barua pepe huna haja ya kufikiri juu ya sehemu mtu aliko America, Asia na kwingineko,
tatizo la tofauti ya muda kuwa pengine huenda kule ni asubuhi, au usiku wa manane hivi sasa kama ilvyo kwa simu na njia nyinginezo za mawasiliano halipo.
Hivyo barua pepe hazina kikwazo chochote kile.

kuna ushahidi pia kuwa barua pepe inakidhi haki za binadamu kuwa huru na kuwa na uwezo wa kuwasiliana pasipo kuweka mipaka. Pia ni ya manufaa kwa wananchi wa hali na rika zote.


Anuani pepe (E-mail):

Anuani pepe ni nini? Anuani pepe ni anuani inayokuwezesha kupokea na kutuma ujumbe kupitia mdahalishi/kipeperushi.

Anuani pepe hufunguliwa kwenye tovuti. Namna ya kujiandikisha na kufungua anwani pepe kwenye tovuti.


Anuani ya barua pepe huwa ni bure na hamna malipo yoyote katika kufungua wala kuendelea kuitumia na huwa ni yako daima.

Ilikuweza kutuma barua pepe inakubidi uwe na anuani pepe na ndipo kwa kutumia anuani yako hiyo wewe utaweza kumwandikia barua pepe mtu mwingine.

Ni ukweli usiopingika kuwa huwezi kutuma barua pepe hadi uwe una anuani yako.

Unapotaka kufungua anuani ya barua pepe unalazimika kuchagua tovuti mojawapo ya zile ambazo zinatoa huduma ya barua pepe.

Kuna tovuti maarufu na zilizozoeleka kwa kutoa huduma za barua pepe mfano; www.yahoo.com, www.hotmail.com, www.raha.com, www.newafrica.com, www.cats-net, www.37.com na nyingine nyingi.

Maelezo yakufuata wakati wakufungua anuani ya barua pepe katika Tovuti ya yahoo.

Mara baada ya kuandika anuani ya tovuti ya yahoo na kufunguka bonyeza sehemu iliyoandikwa MAIL.

Baada ya kubonyeza mail ukurasa utakao kuja utakuwa kama huu hapa

Mkono wako wa kushoto karibia chini utaona sehemu iliyoandikwa Jiandikishe sasa (Sign up now). Bonyeza hiyo sehemu ili kujiandikisha.

Baada ya kufungu ukurasa huo upande wako wa kushoto tena karibia chini utaona imegawanyika katika sehemu tatu.

Moja ni Free Edition

Mbili ni Custom Edition ($35/year)
Tatu ni Business Edition ($9.95/month).

Chagua sehemu iliyoandikwa free edition kisha bonyeza chini yake palipoandikwa jiandikishe sasa (sign up now). kwa kuwa hizo mbili zilizobaki ni za kulipia.

Baada ya ukurasa unaofuatia kufunguka kinachofuata ni fomu ya kujaza. Fomu hii ina maelezo yanayojitosheleza ila inahitaji uangalifu na kuwa ukiacha sehemu fulani bila ya akuijaza basi hutafanikiwa kupata anuani.

Kujaza fomu

  1. Jaza jina lako la kipekee kwenye kisanduku cha kwanza (Yahoo ! ID)[_________]@yahoo.com, mfano: temup

  2. Namba yako ya siri (password)[__________] mfano:xxxxx (peter). Hii huwa inaonyeshwa kwa alama xxx kila unapoiandika ili mtu asiijue.

  3. Andika upya namba yako ya siri (Re-type password)[_________]. Hapa unarudia kuandika tena ile namba yako ya siri ili kuthibitisha kuwa unaikumbuka na umeishika vyema.

  4. Endapo utaisahau namba yako ya siri itabidi ujibu maswali kadhaa ili upewe tena upya. Chagua swali mojawapo katika kisanduku hapo chini ili ukipoteza namba yako ya siri uweze kuulizwa na ukipata upewe. katika kijisanduku kilichoandikwa chagua swali ujibu, (select question to answer)[____________]

      Maswali ni kama ifuatavyo:
    • Mnyama wako wa kufugwa anaitwaje?(What is your pet's name?)
    • [________]

    • Shule yako ya kwanza ilikuwa inaitwaje? (What was the name of your first school?)[_________]

    • Nani alikuwa shujaa wako wakati wa utotoni? (Who was your childhood hero?)[_______]

    • Wewe hupendelea kufanya nini kupitisha mda? (What is your favourite past-time?)[________]

    • Ni timu gani ya mchezo uipendao kila wakati? (What is your all-time favourite sports team?)[__________]

    • Jina la kati la baba yako ni nani? (What is your father's middle name?)[_________]

    • Nani au kitu gani unachokichukulia kilikua kinakupa bahati wakati ukisoma sekondary? (what was your high school mascot?)[__________]

    • Gari lako au Pikiki yako ya kwanza ilikuwa imetengenezwa na nini? (what make was your first car or bike?)[____________]

    • Kwa mara ya kwanza mlikutana wapi na mchumba wako? (where did you first meet your spouse?)

  5. Jibu lako (Your answer)[__________]

  6. Siku ya Kuzaliwa (Birthday) chagua moja kwenye kisanduku kati ya Januari[__]hadi Desemba (select one)[_______]mfano kama umezaliwa Aprili chagua APRIL kisha andika tarehe (date)[___] kwenye kisanduku cha kati na kisanduku cha mwisho andika mwaka (year)[_____](mwezi[_]siku[_]mwaka[_]/month[_]day[_]year_).

  7. Anuani pepe uliyonayo hivi sasa (Sio lazima) (Current e-mail address optional)[_______]

  8. Lugha na yaliyomo Chagua moja _kiingereza cha America, kiingereza cha Canada, kiingereza cha Wingereza n.k. (Language and content-USA English, CANADA English U.K. English, e.t.c.)

    Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa aina ya lugha huathiri namna anuani itakavyo onekana mfano: temup@yahoo.co.uk__temup@yahoo.co.ca na temup@yahoo.com

  9. Namba inayowakilisha nchi yako au namba ya posta ya nchi yako (zipcode/postal code)[______]

    Hapa jaza tarakimu tano mfano 02255 au 12345 kodi ya posta hatuna Tanzania na nchi nyingine nyingi hazina zipkodi wala kodi ya posta na nchi ambazo wanatumia sana ni Uingereza na Marekani ila ili upate aniuani yako na usikiuke mashariti yao wewe andika namba zozote tano 23234 au 02255, kodi ya posta 255

  10. Jinsia (Gender)[_______]kiume/kikeKazi unayoifanya (Industry)[_______]mfano:Mwalimu/mwanafunzi (Education), Msanii/muijizaji (Artist/Actor)

  11. Cheo/nafasi uliyonayo kazini kwako (Title)[________]Mfano:Meneja/Mkurugenzi/Mchambuzi/karani/mwalimu (Manager/Director/Analyst/Clerk/Teacher)


Chagua vitu mbalimbali ambavyo ungependa uwe unatumiwa habari zake kwenye anuani yako hiyo. Hizi habari sio lazima ila nikama wewe mwenyewe tu unataka.


  • Biashara (Business)[___]

  • Viburudisho (Entertainment)[___]

  • Muziki (music)[___]

  • Afya (health)[___]

  • Safari (travelling)

  • Andika neno lililopo kwenye hicho kisanduku hapo chini kwenye nafasi uliyopewa pembeni yake; [siri] [secret] [____]

  • Kisha bonyeza neno linalofuata hapo chini

    Tuma hii Fomu (Submit this Form)

    .

    Baada ya hapa utaletewa ukurasa mwingine ukiwa na maneno yafuatayo

      Tafadhali jaza upya sehemu zilizoandikwa kwa rangi nyekundu (Please re-enter the entries labeled in red)

    • Jina lako la kipekee (yahoo!ID)__mtandaobora ( huu ni mfano)

    • Namba yako ya siri (password) [imefichwa/notshown]


    1. Uraia wako [nchi yako] (Residence:) chagua [_________] mfano Uganda/kenya/Tanzania/Somalia n.k.

    2. Namba inayowakilisha nchi yako au namba ya posta ya nchi yako (zipcode/postal code)[______]Tanzania hatuna wewe jaza tarakimu zozote tano tu kodi ya posta andika hii japo sio ya ukweli kwani hatuna ila hii huwa inakubali 255.

    3. Kisha bonyeza neno linalofuata hapo chini

      Tuma hii Fomu (Submit this Form))

      .

      Baada ya hapa utaletewa ukurasa mwingine ukiwa na maneno yafuatayo

    Kujiandikisha kumekamilika karibu kwenye barua pepe kupitia yahoo!. (Registration Completed Welcome to yahoo mail

    Jina lako la kipekee ni (your yahoo ID is :)mtandao wetu

    Anuani yako mpya ya barua pepe ni (you new yahoo!mail address is ) mtandaowetu@yahoo.com.)

    .

    Baada ya hapa mwisho wa ukurasa kutakuwa na maneno yafuatayo

    Endelea kwenye anuani yako ya yahoo (Continue to yahoo mail) Pia utapaswa kujua namna ya kusoma barua pepe zako na kujibu barua pepe zako. Kusoma barua Pepe
    kisha kuandika


    [Back to top ][Rudi nyuma(Back)Mdahalishi2]
    [Endelea (Next)Outlook][ Rudi Mwanzo wa Tovuti]