Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

Mafunzo Juu ya Mtandao wa Mdahalishi/Kipeperushi(Internet)

Utangulizi kuhusu Mtandao wa Mdahalishi/Kipeperushi:
(Introduction to the Internet).





Mtandao wa kipeperushi/Mdahalishi (internet) ni Mtandao wa Dunia nzima wenye mfumo ambao unatuwezesha sisi, yaani watumiaji, kuhusianisha, kutafuta, kuwasiliana, na kuelimishana.

Kuingia katika mtandao hutuwezesha sisi kutafuta habari mbalimbali zilizohifadhiwa kwenye tarakilishi/kompyuta sehemu nyinginezo duniani pote.

Ninauchukulia au kuona mtandao huu kama mfumo wa barabara, njia na madaraja huru kwa mtu yeyote kupita au kuyatumia yaani kwa watumiaji wote ambao wameunganishwa kwenye mtandao huu.

"Mtandao wa Mitandao" (Networks of networks) ni mtandao mkubwa unaounda mtandao wa kipeperushi (Mdahalishi). Mtandao wa Mdahalishi/kipeperushi (kompyuta) wenyewe hauhifadhi habari zozote.

Ni maelezo yasiyo sahihi kusema kuwa kitu fulani kilipatikana kwenye mtandao wa kipeperushi/Mdahalishi (internet). Inafaa kusema kuwa kitu fulani kimepatikana kupitia au kwa kutumia mtandao wa kipeperushi (internet).

Mtandao wa kipeperushi uligunduliwa na idara ya ya ulinzi ya Amerika mnamo miaka ya sitini. Hii ilikuwa kwa ajili ya kuunganisha vyuo vikuu vya kijeshi na vitengo vya ulinzi pamoja wakati wa matukio ya vita.

Katika siku za awali, kile tunachokiita matandao wa kipeperushi (internet) kwa sasa kilijulikana kama ARPANet Mtandao wa hali ya juu wa miradi ya utafiti (Advanced Research Projects Agency Network).

Taasisi za elimu zilijiunga kwenye mtandao wa kipeperushi (internet) Band-Wagon mwanzoni mwa miaka ya 1980. Kwa mujibu wa mtandao wa Global Reach inakadiriwa watu milioni 322 wanatumia mtandao wa kipeperushi (internet).

Rudi juu (Back to Top)


Matumizi muhimu ya Mtandao wa Mdahalishi/ kipeperushi (internet). (Using The Internet)

Webu brausa (Web Browser)

Webu brausa (Web Browser)
- ni maazimio ya mambo ya kufanya ambayo unayatumia kuangalizia matandao wa kipeperushi. Kuna aina mbili kuu za brausa, ambazo ni Microsoft Internet Explorer, na Netscape Navigator.

Tunaweza kutumia mojawapo ya hizi mbili kwa ajili ya (surfing) kubofya/kuangalia mtandao wa kompyuta.


Hizi ni picha za Brausa







Namna ya kwenda mbele na kurudi nyuma (forward and back icons) wakati wa kubofya (surf)kwenye kipeperushi.Tazama hii michoro hapa chini kwa makini kisha utapata kuelewa namna ya kwenda mbele na kurudi nyuma.







Tovuti (Website) na Ukurasa wa Tovuti (Webpage).

Tovuti ni (A Website) sehemu ndani ya mtandao wa kompyuta ambako kuna kurasa zaidi ya moja za mtandao kurasa za mtandao (Webpages) . kwa mfano "Mtandaowetu" ni Tovuti (Website).

Ilihali "kipeperushi" (Internet) unaoutizama sasa ni moja ya kurasa zake. Ukurasa wa Tovuti(Webpage).

Anuani ya Tovuti (URL)

Ni anuani ya tovuti au ukurasa wa tovuti. Mfano anwani ya tovuti
ya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam ni http://www.udsm.ac.tz.

Hii ndiyo anwani ambayo unapaswa kuiandika kwenye sehemu ya kuandika anuani za tovuti (address bar) juu ya Internet Explorer ilikufungua tovuti ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam.



Sehemu ya kuandikia anuani ya Tovuti.
Anuani ziko katika miundo tofautitofauti kama ifuatavyo:


My table
Aina za tovuti Kimataifa Tanzania Uingereza Afrika Kusini
Kampuni comco.tzco.ukco.za
Shirika org or.tzor.ukor.za
Serikaligovac.tzac.ukac.za
Vyuo na taasisi za Elimu edu go.tzgo.ukgo.za

Mifano ya nchi nyinginezo ni kama vile


seSweden
auAustraralia
keKenya
caCanada
ugUganda

Sehemu ya nchi nyinginezo maneno kama vile se, ke, za, na uk ni badala ya yale yanayotumiwa na Tanzania.

  1. www.udsm.ac.tz------ UDSM--- -neno--ac--linamaanisha ni tovuti ya kitaaluma (academic/academics) Ya Tanzania


  2. www.ucc.co.tz---------UCC--hapa----co--- inamaanisha kampuni/ya kibiashara (company) ya Tanzania


  3. www.raha.com----RAHA--com--mara nyingi husimama kuamaanisha yoyote.


  4. www.mtandaowetu.org-----org-------inasimama kumaanisha Shirika (organization).
  5. www.oxford.edu---------------OXFORD---------edu------------pia inamaanisha elimu (education).

  6. www.go.tz-------------TANZANIA-------tz-------inamaanisha nchi (Tanzania) .

  7. www.spray.se--------------------------se---------inamaanisha nchi (Sweden) .
    SPRAY---
  8. www.nation.co.ke----------Nation----------------ke------------- inamaanisha nchi (Kenya) .

Hizo ni baadhi tu na ambazo ni muhimu kuzijua. nyingine utazijua kwa kadri ya mwendelezo wa mafunzo na pia waweza kujitafutia mwenyewe.



[Rudi juu (Back to Top)][Endelea (next)-Madahalishi2]
[Rudi Nyuma (Back)-Windows3]